Judith ateuliwa kuwa Waziri Mkuu DRC

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:15 AM Apr 02 2024
 Waziri Mkuu DRC, Judith Suminwa Tuluka.
PICHA: DAILY TRUST
Waziri Mkuu DRC, Judith Suminwa Tuluka.

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi, amemteua Waziri wake wa Mipango, Judith Tuluka Suminwa kuwa Waziri mkuu.

Judith anakuwa mwanamke wa kwanza kwa Taifa hilo kuwa Waziri Mkuu akichukua nafasi ya Jean-Michel Sama Lukonde aliyejiuzulu wiki mbili zilizopita.

Lukonde (46), aliyekuwa madarakani kwa miaka mitatu, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu Februari 15, 2021 baada ya muungano wa Rais wa zamani, Joseph Kabila na ule wa FĂ©lix Tshisekedi kuvunjika.

Hata hivyo, uteuzi wa Judith sasa unamaliza utata wa Serikali yake iliyorudi madarakani baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 20, 2023 na kumpa ushindi.

Tshisekedi alikuwa akitafuta kuungwa mkono bungeni na vyama vingine vyenye wabunge wengi kabla ya kuteua waziri mkuu na kuunda serikali.