Wanawake zaidi 1,000, wenye ulemavu 110 kunufaika mradi wa PPP

By Grace Mwakalinga , Nipashe
Published at 02:58 PM Nov 05 2024
Baadhi ya wanawake wanaonufaika na mradi wa kujikwamua kiuchumi na utunzaji mazingira kupitia Mradi wa PPP unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Transform Trade kwa kushirikiana na Shirika la Tangsen katika Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani,wakianika mazao
Picha: Grace Mwakalinga
Baadhi ya wanawake wanaonufaika na mradi wa kujikwamua kiuchumi na utunzaji mazingira kupitia Mradi wa PPP unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Transform Trade kwa kushirikiana na Shirika la Tangsen katika Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani,wakianika mazao

ZAIDI ya wanawake 1,000 na watu wenye ulemavu 110 katika Wilaya ya Rufiji na Kisarawe, mkoani Pwani, wamepata fursa ya kujiimarisha kiuchumi na kutunza mazingira, kupitia mradi wa PPP (People, Planet, and Prosperity), unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Transform Trade kwa kushirikiana na Shirika la Tangsen.

Mradi huo  umejikita katika kutoa mafunzo  kwa wakulima, wafugaji na wajasiriamali namna ya kujikwamua  kiuchumi na uhifadhi wa mazingira kwa ajili ya kuboresha hali ya maisha.

Kupitia mradi huo, wanawake na wenye walemavu wamepatiwa mafunzo yenye tija  katika kilimo cha mazao ili kuongeza  thamani kwenye alizeti, mbogamboga, miti ya matunda, ufugaji wa kuku na nyuki.

Kwa mujibu wa Sebastian Mahenge, Ofisa Biashara na Masoko wa  Shirika la Kimataifa la Transform Trade, amesema unasaidia wanajamii kuimarisha shughuli zao za kiuchumi kwa kutumia mbinu rafiki za kisasa na endelevu kwa ajili ya kutunza mazingira.

Amesema mbinu hizo ni pamoja na  kuwaunganisha katika vikundi vya kiuchumi kwa ajili ya kupata masoko  hatua inayowapa fursa ya kuuza bidhaa zao kwa bei nzuri na hivyo kuongeza kipato.

Amefafanua kuwa lengo la mradi lilikuwa kuwafikia wakulima 2,200, lakini hadi sasa tumewafikia wakulima 2,548, kati yao 1,308 ni wanawake na 1,240 ni wanaume.

Ameongeza kuwa mradi ulikuwa na lengo la kuwafikia wakulima 100 wenye ulemavu, lakini umewafikia wakulima 110, na wakulima wote 2,548 wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kiuchumi, vinavyowawezesha kushirikiana katika kukuza uzalishaji na kuboresha maisha yao kiuchumi.

1

“Tumekusudia kuinua kipato chao na wakati huo huo kuhakikisha mazingira yanatunzwa, wanapata ujuzi wa kisasa kutoka kwa wataalam wa kilimo na ufugaji, pamoja na mbinu bora za kulinda mazingira," amesema Mahenge.

Ameongeza kuwa mradi huu pia unalenga kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uchomaji wa mkaa, ambao umekuwa tatizo kubwa katika wilaya za Kisarawe na Rufiji.

Mradi wa PPP ulianza mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika Machi 2025, kwa kushirikiana na Shirika la Tansing, ambalo lina utaalam katika nishati na jinsia, Transform Trade inatekeleza mradi huu kwa lengo la kuwezesha jamii kupata kipato endelevu huku wakiimarisha uhifadhi wa mazingira yao.

Amesema PPP inachangia ustawi wa jamii kwa kuwapa wanawake na walemavu maarifa na nyenzo zinazowawezesha kuboresha maisha yao huku wakihifadhi mazingira, unawaandaa kuwa washiriki wa maendeleo endelevu kwa vizazi vijavyo, kwa kujenga misingi thabiti ya kiuchumi na utunzaji wa mazingira.
Mwisho. mazingira," amesema Mahenge.

Mratibu Mradi PPP kutoka Shirika la Tangsen wilaya za Rufiji na Kisarawe, Leonard Pesambili, amesema wamezingatia masuala ya kijinsia katika kutekeleza ili kuongeza  idadi ya wanawake na wenye ulemavu  na kunufaika fursa mbalimbali zinazopatikana katika maeneo yao.

Rahma Mnara, Mwalimu wa Kilimo na Mifugo kutoka Rufiji, amesema wamefanikiwa kuwajengea uwezo wakulima kuongeza thamani ya mazao yao kwa kukausha kwa kutumia teknolojia ya umeme jua (solar dryer).

4