Maafisa wa Umma wote waliorekodiwa na Baltasar kufukuzwa kazi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:25 PM Nov 05 2024
Baltasar Ebang Engonga (54).
Picha:Mtandao
Baltasar Ebang Engonga (54).

Makamu wa Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mangue amesema Serikali ya Nchi hiyo itawatimua kazini maafisa na watumishi wote wa Umma ambao ni miongoni mwa Wanawake zaidi ya 400 waliorekodiwa wakifanya mapenzi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Upelelezi wa Fedha (ANIF) la Nchini humo, Baltasar Ebang Engonga (54).

Ebang, ambaye ni baba wa watoto sita, amekamatwa kwa kosa la kujirekodi akifanya mapenzi na zaidi ya wanawake 400, wakiwemo wake wa viongozi wa juu serikalini na maafisa wa umma.

Taarifa zinaeleza kuwa video hizo zilirekodiwa katika maeneo mbalimbali, ikiwemo ofisi za serikali na nyumbani kwake. 

Wanawake hao, baadhi wakiwa wake za viongozi, ndugu wa viongozi wa juu serikalini, na maafisa wa ngazi ya juu, walionekana kuridhia kurekodiwa.

Wengine walioonekana wakifanya mapenzi na Ebang kwenye video hizo ni Mke wa Mlinzi wake (Bodyguard), Mke wa Mchungaji wake, Wake wa Mawaziri kadhaa wa Nchi hiyo, Mke wa Mjomba wake ambaye ni Mjamzito, Marafiki 15 wa Mdogo wake wa kike na Wanawake wengine mbalimbali ambapo imeelezwa wote hao walionekana kuridhia video hizo kurekodiwa.