MBUNGE wa Viti Maalum (CHADEMA), Halima Mdee amesema vijana wengi hivi sasa wanaumwa ugonjwa wa figo kutokana na matumizi ya pombe kali zenye sumu zimesambaa maeneo mbalimbali nchini na zinauzwa kwa bei ndogo.
Akiuliza swali bungeni leo, amehoji lini serikali itaanza msako mahsusi kuondoa pombe hizo nchini ili kuokoa kizazi cha sasa na kijacho.
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Godwin Mollel, akijibu swali hilo, amesema pombe zinasababisha madhara mengi na kuwaomba wabunge kuhamasisha wananchi kuishi maisha salama na kuahidi watashirikiana na sekta zingine kuja na mkakati wa kukinga jamii na ugonjwa huo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED