WAJASIRIAMALI wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wametakiwa kuhakikisha wanakuwa wabunifu na kuongeza ujuzi ili kutengeneza bidhaa zenye ubora zaidi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Tanzania jijini Juba, Sudan Kusini ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maonesho ya 24 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu Nguvu Kazi au Jua Kali yanayoendelea jijini humo yakiongozwa na kauli mbiu isemayo.
"Kukuza Ubunifu wa Kipekee na Maendeleo ya Ujuzi miongoni mwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Afrika Mashariki."
Amesema kauli mbiu inahamasisha nchi wanachama wa jumuiya hiyo kutambua na kuthamini suala la kukuza na kuongeza ujuzi na ubunifu kwa wajasiriamali ili kuongeza tija na faida katika utengenezani wa bidhaa zao.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED