Jamii za wafugaji zabadili mtazamo kuhusu kilimo

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 03:02 PM Oct 11 2024
Mkulima Mathayo Olonyoke, akitolea majani katika shamba lake la mikunde.
Picha Maulid Mmbaga.
Mkulima Mathayo Olonyoke, akitolea majani katika shamba lake la mikunde.

JAMII za wafugaji hasa za maasai wanaoishi katika Wilaya ya Simanjiaro mkoani Manyara wamesema kwa sasa kilimo na ufugaji vyote ni vitu vyenye thamani kwao na kwamba kwa zaidi ya miaka 20 wamekaa na maofisa kilimo ili kupewa mbinu mbalimbali za uzalishaji.

Hayo yamebainishwa leo baada ya waandishi wa habari kufika katika kijiji cha Orkirung'urung'u Tarafa ya Naberera, wilaya ya Simanjiro mkoni Manyara kutembelea mashama darasa kwa ufadhili wa Taasisi ya Uendeshaji wa Mifumo ya Masoko ya Kilimo (AMDT) kwa lengo la kujionea maendeleo ya wakulima wanaofadhiliwa chini ya mradi wa VACS unaojumuisha teknolojia ya umwagiliaji kwa njia ya matone.

Mathayo Olonyoke, ambaye miongoni mwa wafugaji waliogeukia kilimo, na mkazi wa kijiji hicho amesema kutokana na mafunzo wanayopatiwa na taasisi mbalimbali kama AMDT wakishirikiana na kampuni ya mbolea ya Beula, sasa imefika mahali wanaona kuwa kilimo ni bora kama ufugaji.

"Kwahiyo hatutaki shamba ikanyage mifugo, wala mifugo ikanyage shamba, tumeshapiga vita mambo ya kukata ng'ombe miguu hatutaki ikila mazao tunata ofisa kiliko afanye tathimini alafu ichukuliwe hatua kwa haraka sana ilipwe mazao kama fidia," amesema Olonyoke.

1

"Tunalinda sana na tumeshasema hatutegemei mifugo yenyewe sasa hivi, kwahiyo kilimo nafikiri ni uhai wetu na ni bora kama ufugaji, na hatutegemei kuona mifugo ikienda kukanyaga shamba, na maeneo mengi tuliyootesha mazao hatujaweka uzio lakini hakuna mtu yoyote anaeweza kuthubutu kukanyagisha Ng'ombe," amesema Olonyoke.

Pia Olonyoke, ameeleza kuwa kilimo cha kisasa cha umwahili ambacho amekuwa akijihusisha nacho kwa zaidi ya miaka 20, amepata mafanikio mengi ikiwemo kuchochea hali yake ya kiu humi, uhakika wa chakula, na kusomesha watoto wake ambao wengine kwa sasa wako chuo kikuu.
2