Muhimbili kurejesha tabasamu wenye ulemavu wa kuzaliwa, ajali

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 02:14 PM Oct 11 2024
Bingwa wa Upasuaji Rekebishi na Upasuaji Urembo kutoka Idara ya Upasuaji huo MNH, Dk. Edwin Mrema.

HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH), imepanga kufanya upasuaji Rekebishi kwa watu wenye ulemavu wa kuzaliwa nao pamoja na waliopata ajali na viungo vyao kuondoa uhalisia wake.

Kambi ya takribani siku 12 inatarajiwa kuanza Oktoba 21 hadi Novemba Mosi, mwaka huu, huku walengwa wakiwa ni wenye matatizo mbalimbali ya ulemavu wa mikono, miguu, sura na sehemu mbalimbali za mwili kutokana na ajali, moto ama kuzaliwa.

Bingwa wa Upasuaji Rekebishi na Upasuaji Urembo kutoka Idara ya Upasuaji huo MNH, Dk. Edwin Mrema, ameyasema hayo leo, jijini Dar es Salaam, akizungumza na Nipashe kuhusu kambi hiyo.