Akiba Commercial Bank Plc yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:23 PM Oct 09 2024
Akiba Commercial Bank Plc yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
Picha: Mpigapicha Wetu
Akiba Commercial Bank Plc yaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja

Benki ya Akiba Commercial Plc imewashukuru wateja wake kuungana nao katika safari hii ya kutoa huduma bora zaidi za kibenki ambazo zinachangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania

Shukrani hizo zimetolewa  leo Oktoba 9,2024 Dar es salaam na  Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Akiba Commercia, Silvest Arumasi katika  Maadhimisho ya Wiki ya huduma  kwa wateja hafla iliyofanyika   tawi la  Ubungo la benki hiyo  na kuhudhuriwa na Wateja  wafanyakazi wa benki , na wawakilishi wa vyombo vya habari.


Mkurugenzi amesema wiki ya huduma kwa wateja  wameifanya kwa namna ya kipekee kwa  kutambua thamani ya wateja kwa kutoa tunzo kwani kufanya hivyo ni  kuonesha ahadi ya benki ya kuendelea kutoa huduma bora.


Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Above and Beyond” ikimaanisha kwenda zaidi ya matarajio, kauli ambayo inakusudia kuhamasisha utoaji wa huduma bora zaidi kwa wateja.

Mtendaji wa benki ya Akiba Commercia, Silvest Arumasi.

“Niwashukuru wateja wetu kutuchagua kuwa washirika wenu wa kibiashara kwani bila nyinyi , tusingeweza kufikia mafanikio haya tunayojivunia leo hivyo wiki hii ni maalum kwa ajili yenu, tunathamini na  kutambua mchango wenu ” amesema  Arumasi


Hata hivyo Akiba Commercial  benki imefanya maboresho yaliyofanyika katika huduma za kidijitali za benki, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za ACB Mobile na Akiba Wakala kwa kuzingatia mahitaji ya wateja. 


Akiba Commercial benki inafanya   huduma mpya ya Internet Banking inayopatikana kwa wateja binafsi, makampuni makubwa, na taasisi mbalimbali, kama sehemu ya mkakati wa mabadiliko ya kidijitali wa benki hiyo kwa kauli mbiu “Twende Kidijitali.”“Kwa kuzingatia mabadiliko ya haraka ya kiteknolojia.

 "Mwaka 2024 tumeamua kuupa  jina la Mwaka wa Kidijitali,’ na tumejidhatiti kuwafikishia huduma za kibenki kwa njia ya kisasa zaidi kupitia mifumo yetu ya kidijitali,” ameongeza Arumasi.


Maadhimisho ya  wiki hii, Akiba Commercial Bank inafanya shughuli mbalimbali katika matawi yake yaliyopo Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya, na Dodoma ili kuwapa wateja fursa ya kuona na kushiriki katika maboresho yanayoendelea kufanywa.

3

 Aidha Benki itaendelea  kukusanya  maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja ili kuboresha bidhaa na huduma zake kwa ujumla.“Wiki hii siyo tu kwa ajili ya sherehe, bali ni ahadi yetu ya kuendelea kuboresha na kutoa huduma bora ambazo zitazidi matarajio yenu,” amesema Arumasi

4