OYA yalaani tukio lililopelekea kifo cha mteja wake

By Faustine Feliciane , Nipashe
Published at 10:59 PM Oct 09 2024
Magari ya Kampuni ya Oya.
Picha: Mtandao
Magari ya Kampuni ya Oya.

KAMPUNI ya OYA imelaani kitendo cha maafisa wake kutumia nguvu wakati wakidai madeni na kupelekea kumpiga mteja wake Juma Mfaume na kupelekea kifo chake.

Kampuni hiyo imesema tukio hilo lililotokea Oktoba 7, 2024, Mlandizi mkoani Pwani si utaratibu wa kampuni hiyo katika kudai madeni yake.

Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo imesema itashirikiana na mamlaka husika katika kufanikisha uchunguzi wa tukio hilo.

"Kampuni inazingatia staha na sheria katika kufuatilia madeni yake, tunalaani kwa nguvu zote tukio hili na tutatoa ushirikiano kwa Mamlaka kwenye uchunguzi", imesema sehemu ya taarifa hiyo.