Akiba Benki yazindua kampeni "Tupo Mtaani Kwako"

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:26 PM Sep 21 2024
Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango
Picha: Mpigapicha Wetu
Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango

Taasisi za kifedha hazina budi kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi kwa kuwasogezea karibu ili kusaidia kupunguza adha ya kutumia muda mwingi kufuata huduma umbali mrefu na kuchelewa kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Wito huo ametolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo Biashara Benki ya Akiba, Danford Muyango  wakati akizindua rasmi kampeni ya “Tupo Mtaani Kwako” katika tawi la Kijitonyama la benki hiyo, Letsya Tower.

Amesema wapo mtaani kila mahali wakitoa huduma ikiwemo elimu ya mikopo, jinsi ya kutumia huduma za kidigital VISA card,ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking.

1

”Tumezindua rasmi program yetu ya "Tupo Mtaani Kwako" kupitia timu yetu bobezi ya mauzo  sasa tunakufika popote ulipo nchi nzima  kupitia timu yetu ya mauzo kupata huduma zetu za kufungua akaunti, elimu ya mikopo pamoja na jinsi ya kutumia huduma zetu za kidijitali za VISA card, ACB Mobile, Akiba Wakala na Internet Banking" amesema Muyungo

Muyango amesema Program hiyo inaenda sambamba na kampeni ya Road show ya kutoa utambulisho kwa timu ya “Tupo Mtaani kwako” katika vitongoji na mitaa mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam.
2