Malezi bora ya mjamzito yazingatiwe kulinda afya ya mama na mtoto
UKUAJI wa mtoto kibaiolojia huanza kuhesabiwa tangu siku ya kwanza mimba inapotungwa. Wataalamu wa afya wanazitaja siku 1,000 za ukuaji huo kuwa muhimu zaidi kwa afya ya mama na mtoto.