MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara, John Heche amewataka wanachama wa chama hicho kutokuingia kwenye kile alichokiita mtego wa kukipasua chama.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho wa Kanda ya Kaskazini, mkoani Arusha Heche amesema zipo juhudi zinafanyika ili kukipasua chama hicho na kukidhoofisha kutokuendelea na ajenda zake muhimu.
“Walikuwa wanategemea chama hiki kitakufa ,tutatoka Mlimani City tumekufa, tumewaonesha nchi nzima watu hawakulala wanaifuatilia Chadema kwa jinsi watu walivyokuwa na matumaini na sisi” amesema Heche
“Kuna watu wachache ambao mirija yao imekatwa baada ya viongozi wapya kuingia madarakani hao ndio wana kinyongo wanataka watuletee mgogoro na nataka nitumie nafasi kuwaambia kwamba we are not weak (sisi sio dhaifu) hatutavumilia hayo mambo” amesema Heche
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED