Maombi ya dhamana ya Dk. Slaa yatinga Mahakama ya Rufaa kwa hati ya dharura

By Imani Nathaniel , Nipashe
Published at 10:26 PM Feb 21 2025
Maombi ya dhamana ya Dk. Slaa yatinga Mahakama ya Rufaa kwa hati ya dharura
Picha: Maktaba Nipashe Digital
Maombi ya dhamana ya Dk. Slaa yatinga Mahakama ya Rufaa kwa hati ya dharura

Maombi ya dhamana ya Dk. Wilbroad Peter Slaa wakati rufaa yake ikiendelea kusubiriwa (bail pending appeal) yamesajiliwa rasmi katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa hati ya dharura, ikiwa ni Maombi Nambari 6889441 ya mwaka 2025, katika Masijala ya Dar es Salaam.

Mawakili wa Dk. Slaa wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakikumbusha kuwa mnamo tarehe 10 Januari 2025, Dk. Slaa alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Beda Nyaki, akikabiliwa na shtaka moja la kuchapisha taarifa ya uongo kwenye mtandao wa X (zamani Twitter). 

Hata hivyo, dhamana yake ilizuiliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa madai ya kutokamilika kwa uchunguzi na sababu za kiusalama.

1

"Kwa sasa, kinachosubiriwa ni Mahakama ya Rufani kupanga taratibu za usikilizwaji wa shauri hili, ambalo limezua gumzo kutokana na mazingira yaliyopelekea Dk. Slaa kunyimwa dhamana kwa kosa lenye dhamana. Ni imani yetu kwamba Mahakama ya Rufani itasimamia vyema wajibu wake wa kikatiba na kutegua kitendawili hiki," amesema Wakili Mwasipo.

Aidha, amebainisha kuwa tayari Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameshapokea nakala za maombi hayo kwa ajili ya hatua zinazofuata.
2