Pongezi Wasira, ana majukumu mazito kufanya ndani ya CCM
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana walimchagua kwa kishindo mwanasiasa mkongwe, Stephen Wasira, kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara. Wasira amechaguliwa kuziba nafasi ya Abdulrahman Kinana aliyeachia ngazi Julai, mwaka jana.