Man Utd inamtaka Delap wa Ipswich

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:47 PM Feb 19 2025
Liam Delap
Picha: Mtandao
Liam Delap

MANCHESTER United, wanamtaka mshambuliaji wa timu ya vijana ya England chini ya miaka 21 kutoka Ipswich Town, mwenye thamani ya Pauni milioni 40, Liam Delap mwenye miaka 22.

Delap, ambaye alitoka timu ya vijana ya Manchester City, amefunga mabao 10 katika ligi kuu ya England msimu huu na pia anaswakwa na Chelsea pia. 

Liverpool iko tayari kumtoa mshambuliaji wake Mruguay, Darwin Nunez, 25, pamoja na fedha, ili kumnasa mshambuliaji Msweden, Alexander Isak, 25, kutoka Newcastle, ambaye ana thamani ya pauni milioni £40m100m. Isak amefunga mabao 17 kwenye ligi kuu England msimu huu.

Alexander Isak
Arsenal na Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji wa Ufaransa anayekipiga Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 22, kama mbadala wa Isak.

Chanzo: BBC