Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema maboresho yatakayofanyika kuanzia Februari 22 hadi Februari 28, 2025 hayatofanyika kwa siku sita mfululizo na hayatowaathiri Wananchi hivyo waondoe hofu.
Taarifa ya Tanesco imeeleza kuwa: "Tutakuwa na maboresho ya miundombinu yatakayofanyika katika Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusafirisha umeme cha Ubungo ambayo yanaweza kuathiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti kwenye baadhi ya maeneo ya Zanzibar, Dar na Pwani, tunapenda kuwatoa hofu wananchi kuwa maboresho haya hayatakuwa kwa siku sita mfululizo na hayatawaathiri Wananchi kwa muda wote"
Tanesco imesema inafanya kila jitihada kuhakikisha athari zitakazotokana na maboresho hayo kuwa za kiwango cha chini kadri iwezekanavyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED