Waziri Kombo atembelea watengeneza ‘drones’ za kilimo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 10:52 AM Feb 21 2025
Waziri Kombo atembelea  watengeneza ‘drones’  za kilimo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri Kombo atembelea watengeneza ‘drones’ za kilimo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo amefanya ziara katika Kampuni ya ABZ Innovation inayojihusisha na uzalishaji wa ndege zisizo na rubani ‘drones’ zinazotumika katika sekta ya kilimo.

Katika ziara hiyo Waziri Kombo alipokea wasilisho kuhusu ndege hizo zinazozalishwa na kampuni ya ABZ Innovation ambazo zaidi hutumika katika kumwagilia mashamba, kunyunyizia dawa mashambani, kupuliza dawa ya kuua wadudu waenezao magonjwa kama vile mbu ili kupunguza na kudhibiti ugonjwa wa malaria.

Uwezo wa ndege hizo hutofautiana huku nyingine zikiweza kubeba lita 30 za maji na kumwagilia zaidi ya hekta 24 kwa saa.