Awamu ya Sita ikitekeleza alichobuni Nyerere 1964, kupitia nyenzo MMAM

By Peter Orwa , Nipashe
Published at 07:58 AM Oct 03 2024
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwapa zawadi kinamama waliojifungua katika jengo jipya la ‘Mama na Mtoto’ kwenye Hospitali ya CCBRT, Dar es Salaam, Julai, 2022.
PICHA: MAKTABA
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akiwapa zawadi kinamama waliojifungua katika jengo jipya la ‘Mama na Mtoto’ kwenye Hospitali ya CCBRT, Dar es Salaam, Julai, 2022.

KINADHARIA, kitaifa mwaka 1964 unajulikana kuwa msaafu wa taifa, katika mipango mikuu. Ndio Mpango wa Kwanza wa Maendeleo ya Nchi wa miaka mitano.

Ndani yake ilibeba dhana kuu tatu; mwanzo wa kuingia rasmi nchi na mipango yake mikuu; pili kutimizia nchi mahitaji ya msingi kimaendeleo na kimaisha, kabla ya kukwea juu zaidi kimaendeleo. 

Pia, sura ya tatu ilinuia kuwahamisha Watanzania kujitegemea kwa kuzalisha na kutumia vya kwao, wakihama kutoka uchumi tegemezi wa ‘kuzalisha wasivyotumia na kutumia wasivyozalisha’ na badala yake, ‘kutumia wanavyozalisha.’ 

Nne, iliangalia kupiga maendeleo ya haraka kuwaondoa katika hatua ya uchumi wa chini waliokuwa wakati huo kukosa vitu vya msingi, miaka mitatu baada ya uhuru. 

Daima hadi sasa mipango yote ya maendeleo inaandaliwa ikiwa na unasaba wa moja kwa moja na mpango huo wa 1964-1969. Mpango huo wa kwanza ulizama zaidi katika huduma za jamii na uchumi, hapo kukizungumziwa sekta za Kilimo, Elimu, Afya, na Ustawi wa Jamii. 

Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi kutimu miaka 10 ya Uhuru, 1971 kukawapo Mpango wa Maendeleo wa Pili 1969- 1974, ikiwa na sura ya maboresho zaidi katika huduma na mifumo ya uchumi kupanda ngazi, mathalani, kuwapo viwanda vidogo (jukumu la SIDO- 1973) na vya kuzalisha bidhaa nyinginezo za uzalishaji. 

Katika afya ikifanana sana na elimu, kukachukuliwa hatua za ziada, kutokana na hali ya chini kimaisha kwa umma uliosababisha na mambo kadhaa. 

Hapo kuna upungufu wa zanahati na hospitali, ufahamu duni wa umma katika masuala ya afya, pia katika vifo vya kinamama na watoto na umaskini kwa jumla.  

Ni kipindi hata mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile ya afya -WHO na UNICEF kwa elimu na utamaduni yalihamasika sana kufanya kazi na Tanzania. 

Kupitia uhamasishaji wa umma wakati huo siasa ya Ujamaa ikitawala hamasa ya nchi na iko rasmi zaidi ya miaka mitano, Serikali ya Awamu ya Kwanza ilipigana kuhamasisha afya, huku ikitekeleza miradi yake mingi nchini. 

Ndipo kampeni zake za hamasa kupitia muziki wa dansi bendi kama Morogoro Jazz, zikatunga nyimbo inayohusu afya iliyotamba, wakati huo muziki wa dansi ukiwa katika nafasi yake- burudani ya umma na Radio Tanzania ikitamba kitaifa kufikisha ujumbe mbali. 

Kwa wanaokumbuka wakati huo, kundi la watu wasiovaa viatu walikuwa wengi ikiwamo Dar es Salaam, pia wenye funza miguuni, wanaokunywa maji yasiyochemshwa na wanaojifungulia nyumbani nao walikuwa wengi. 

Sababu ilikuwa wazi, mfumo wa kikoloni haukujali fursa za elimu ya umma, pia za darasani kwa wazawa wengi, ikizingatiwa utawala wa Kiingereza ulijifahamu ni wa kupita tu (non settlers’ colony). 

Ndio maana baada ya uhuru katika nafasi ya kipekee, kampeni na hamasa za serikali hasa katika mpango wa kwanza uliokoma mwaka 1969, Rais Julius Nyerere kwa kutumia marafiki aliomba misaada ya ujenzi wa zahanati, pia, kusomeshwa wataalamu kimataifa. 

Hapo ndipo ikaanzia hadithi ya kundi kubwa la Watanzania kwenda kusomea utabibu ughaibuni, ikiwamo katika vyuo vikuu vya China na Lumumba, katika iliyokuwa Jamhuri ya Muungano ya Kisovieti (USSR). 

Pia Dar es Salaam, ndio katika miaka ya 1960c ukawa mwanzo wa kujengwa zahanati za Mnazi Mmoja, Temeke, Amana na Mwananyamala ambazo sasa ni hospitali kubwa, huku mkoa kama Tanga kuna Zahanati ya Chumbageni, ambayo sasa ni kituo cha afya katika mchakato kama za Dar es Salaam, kuwa hospitali kubwa kimkoa. 

Ndani ya Mpango wa Pili wa Maendeleo, operesheni kama za Vijiji vya Ujamaa (1974) mradi wa afya vilihamasisha sana umma kufikiwa na huduma za tiba na katika mtaala maarufu wa elimu mwaka 1976, ulijumuisha somo la Maarifa ya Jamii katika elimu ya msingi, ukiwa ni mwendelezo wa elimu ya afya shuleni. 

Daima ni mustakabali ulioendelezwa katika Serikali za Awamu ya Pili chini ya Rais Mzee Ali Hassan Mwinyi na Awamu ya Tatu, Rais Benjamin Mkapa kwa kuwasilisha huduma nyingi za kisekta kwa maeneo hayo, wakipokea na kupokezana kijiti kwa mrithi wake. 

MAGEUZI AWAMU IV 

Ilipotimu Julai 2007, Rais Jakaya Kikwete katika dira ileile ya mwaka 1964 na mwendelezo wa kupokezana vijiti tangu Awamu ya Kwanza, kunuia kumfikia kila mtu ngazi ya msingi au chini, akaanzisha Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM). 

Ni mpango uliokuwa na sura ya maboresho, kuimarisha afya ya umma kuanzia juu hadi chini. Ndani ya tafsiri ya Mpango wa Maendeleo wa mwaka 1964-69 na maboresho yake katika mikakati ya Vijiji vya Ujamaa, MMAM ikataka kila kijiji au kitongoji mijini kuwa na zahanati, huku kata kuwa na kituo cha afya. 

Vilevile wilaya inakuwa na hospitali, mkoa hospitali ya rufani, kukawapo hospitali za rufani za kanda kama vile Mbeya na KCMC Moshi na Hospitali ya Taifa Muhimbili, ikiambatana na nyinginezo zenye hadhi kama zake; Benjamin Mkapa (Dodoma), pia Jakaya Kikwete na MOI za Dar es Salaam. 

Mbali na ujenzi wake, pia zikaimarishwa vifaa na watumishi wenye stadi ndani yake. 

AWAMU YA SITA

Katika tafsiri ya msingi ya ‘kuchonga penseli’ kwa kuendeleza aliyoyakuta, baadhi ya miradi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, akianza nayo awamu ya tano alipokuwa Makamu wa Rais na hata kabla ya hapo, ndio inatoa wasifu Tanzania kung’ara hivi sasa katika stadi za afya. 

Sehemu kubwa ya uwekezaji wake,  nywele vipara.  katika Sekta ya Afya inabeba sura ileile ya mwaka 1964; kuwekeza zaidi katika wataalamu, majengo ya huduma za afya na kampeni za uhamasishaji. 

Kuna maeneo amekuwa akiwajibika moja kwa moja, hasa katika huduma zinazohusu ‘mama na mtoto’ mabako hafichi ukereketwa. 

Pia, bajeti kubwa imekuwa ikizama kuendeleza kampeni za elimu afya, wataalamu wa hospitali kubwa kama za JKCI, MNH na Benjamin Mkapa wakipata ujuzi mkubwa ambao uliokuwa haupatikani nchini, mathalan uoteshaji nywele vipara. 

Ni aina ya elimu za muda mrefu na mfupi, kuwa sehemu ya bajeti ya nchi kila mwaka na zao lake ni kwamba, ngazi ya ujuzi nchini kwa Afrika Mashariki na wigo wa Afrika umekuwa juu. 

Kuna umma wa watu wanaofika nchini kupata huduma tiba iliyokuwa inapatikana mbali kama India, huku wataalamu wa nchi jirani wakifika nchini kupata ujuzi na wale wa Tanzania kwenda kutibu na kutoa mafunzo huko. 

Hapo kuna nchi kama vile Malawi, Burundi na Rwanda na kuzalisha aina mpya ya utalii nchini ‘Utalii Tiba.” 

Vilevile, kuna utaratibu maaluma ya wajuzi hao kuzuri katika hospitali ngazi ya mikoa kupeleka ujuzu huo uwafikie umma uliko. Kwa kifupi sasa, Awamu ya Sita unatekeleza ya mwaka 1964 kwa nyenzo ya MMAM.