Wanne wafariki dunia Zanzibar

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 05:53 PM Oct 03 2024
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Richard Mchomvu.
Picha: Mtandao
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Richard Mchomvu.

WATU wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti Mkoa wa Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar, kwa kipindi cha Septemba 6 hadi Oktoba 2, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari leo (Alhamisi), Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Richard Mchomvu, amesema watu watano wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za mauaji yanayohusishwa na wizi.

Amesema matukio hayo yalitokea kwa nyakati tofauti ikiwa ni kwa matukio ya utekaji,wizi na matumizi mabaya ya pombe.

Moja ya tukio hilo ni lililotokea Oktoba 2,2024 katika eneo la Mbuzi ambapo kijana Masaka Juma (40) alimshambulia mkewe kwa kitu chemye ncha kali na kusabisha kifo chake, kisha naye akajinyonga hadi kufa.

Tukio jingine ni kifo cha kijana Ramadhan Iddi Shabani (49) mkazi wa Chumbuni kukutwa, anayedaiwa kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari kwa ajili ya kwenda kumuhoji na kukutwa amefariki dunia katika eneo la Kijichi.

Kuhusu tukio la mauaji la kijana Idarous Masoud Omar (23) mwili wake ulikitwa kando ya barabara Mombasa ukiwa na majeraha tukio hilo linahusishwa na wizi wa pikipiki ambapo marehemu anadaiwa kuwa ameiba.

Tukio jengine ni Kambalagula Mabula (45) mwili wake ulikutwa kando ya barabara ya fuoni ukiwa na majeraha inadaiwa kuwa alikatizwa uhai wake na watu waliompora mali.