SERIKALI imesema kuwa itajenga njia sita katika barabara mbalimbali nchini, ikiwa ni mkakati wa kupunguza ajali ambazo zinaongezeka kila uchao.
Hayo yamesemwa leo, Alhamis na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya mzunguko yenye urefu wa kilomita 112.3 katika jiji la Dodoma inayotarajiwa kukamilika Machi, 2025.
Amesema mpanago wa serikali hivi sasa ni barabara ambazo zitakuwa zikijengwa katika maeneo mbalimbali ya nchi kuwa za njia ya tatu, ili kusadia kupunguza ajali ambazo zimekuwa zitokea.
“Mpango wa serikali hivi sasa ni ujenzi wa barabara kuwa za njia tatu kwenda na kurudi na kuondokana na ujenzi wa sasa magari kupisha katika njia moja hivyo mpango wetu hata hizi barabara ambazo tunazitumia sasa zikibadilishwa zitakuwa za njia tatu ili kusaidi kupunguza ajali nchini,”amesema Bashungwa.
Akizungumzia ujenzi wa mradi huo wa barabara ya mzunguko ya kilimota 112.3, aliwataka makandarasi kumaliza ndani ya muda wa mkataba kwakuwa serikali haitaongeza hata siku moja ya ziada.
“Serikali haitaongeza hata siku moja ya ziada hivyo mnapaswa kukamilisha ndani ya muda wa mkataba na mkandarasi atakaye shindwa serikali itahakikisha kuwa hata pata kazi tena nyingine nchini, kwani kuongeza muda ni kuongeza pesa hivyo serikali hatakuwa tayari kuongeza kiasi chochote cha pesa kwa mkandarasi,”amesema Bashingwa.
Juni 13, 2024, Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali katika mwaka 2024/2025, alisema watu 7,639 walipoteza maisha ndani ya miaka mitano tangu 2019 hadi Mei 2024 kwa ajali za barabarani.
Jumla ya ajali 10,093 zilitokeana kusababisha majeruhi 12,663 huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED