KAMATI ya Sera ya Fedha (MPC) ya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema kushuka kwa bei ya mafuta ghafi kutapunguza mfumuko wa bei.
Hayo ni wa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa leo (Alhamis) na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT) Emmanuel Tutuba.
Amesema bei za bidhaa katika soko la dunia zimeendelea na zinatarajiwa kuendelea kuwa tulivu.
“Katika robo ya mwaka inayoishia Disemba 2024, bei za mafuta ghafi zinatarajiwa kuwa kati ya dola za Marekani 72 hadi 82 kwa pipa, kutokana na ongezeko la uzalishaji,”amesema na kuongeza:
“Hali hii inatarajiwa kupunguza ongezeko la mfumuko wa bei na mahitaji ya fedha za kigeni nchini kwa kuwa bidhaa za mafuta huchangia takriban asilimia 20 ya bidhaa zote zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.”
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED