Waza haya alafu kajiandikishe, asema DC Twange

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 02:12 PM Oct 17 2024
Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lazaro Twange.

“UNA changamoto unataka kukamatwa, nyumba yako inataka kupekuliwa na chochote kile kinachotokea kwenye mtaa wako, yeye ndiyo mtu wa kwanza.Waza vile unataka barua ya kwenda kumdhamini ndugu yako Kituo cha Polisi, yeye ndio mtu wa kwanza. Kwa hiyo hakikisha unajiandikisha ili ukapige kura kwa mtu ambaye ndiyo hasa, atakayekuwa mwenzako wa kukusaidia. …Kutokujiandikisha hutopiga kura na wenzako watakuchagulia kiongozi, au huenda akachaguliwa kiongozi ambaye wewe hukumtaka. Jiandikishe ili uwe na sifa ya kumchagua kiongozi unayemtaka aje akutumikie.” Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lazaro Twange.