Tanzania mwenyeji Mkutano wa Kimataifa wa Nishati 2025

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 03:54 PM Dec 31 2024
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa Ruwangwa leo.
Picha:Mpigapicha Wetu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi wa Ruwangwa leo.

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa ambao umeandaliwa mahususi kwaajili ya uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi duniani.

Imeelezwa kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika Januari 2025 nchini Tanzania, ikielezwa kuwa uamuzi huo umechagizwa na utashi wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa kinara katika uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia Tanzania na Barani Afrika.

Kauli hiyo imetolewa leo Desemba 31, 2024 Wilayani Ruangwa mkoani Lindi na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya hamasa ya matumizi ya  nishati safi mkoani humo, akiwataka watanzania kumuunga mkono Rais Samia kwa kutumia nishati safi.

"Matumizi ya nishati safi ambayo ni Gesi, Umeme pamoja na makaa ya mawe, yanalinda afya ya Watanzania, yanalinda mazingira dhidi ya ukataji wa miti pamoja na kutoa ulinzi kwenye nishati endelevu," amesema Majaliwa.