KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP. Almachius Muchunguzi amesema mikakati ya ulinzi kwa kushirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa kijamii ili kuhakikisha amani inatawala mkoani humo.
Akiongea na vyombo vya habari leo amesema watahakikisha amani inatawala kwenye maeneo muhimu kama barabara kuu, nyumbani za ibada, kumbi za starehe, fukwe za bahari na maeneo mengine yenye mikusanyiko ya watu.
"Katika juhudi za kudhibiti ajali za barabarani, kuanzia Disemba 15 hado 30, madereva 15 wamefungiwa leseni zao kwa makosa mbalimbali, makosa 404 yameripotiwa pamoja na kiasi cha sh milioni 119.625 zimekusanyea kama tozo za papo kwa papo,
"Lakini pia yamekamatwa magari 10 yasiyofaa kutembelea na kuondokewa namba za usajili huku matajiri wa magari hayo kutakiwa kuyarekebisha kabla ya kuruhusiwa kurudi tena barabarani" amesema.
Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama ili kupunguza ajali za barabarani na kuboresha hali ya usalama kwa watumiaji.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED