Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, ameiagiza polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Arusha kumkamata Ofisa Mtendaji wa kata ya Bwawani, Simon Kaaya, baada ya wananchi kudai amekuwa akiuza viwanja vya kijji na kuyakodisha.
Makonda alitoa agizo hilo baada ya kukagua kukakua kituo cha afya ya Bwawani kata ya Bwawani wilayani Arumeru ambapo wananchi walimlalamikia ni chanzo cha migogoro na kuuza mashamba ya kijiji na kuyakodisha kwa Sh 50,000.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Lucas Samwel, amesema aliuziwa kiwanja kwa Sh milioni mbili fedha hizo alikopa kwa riba kwenye kikundi na viongozi wa kijiji walimpatia risiti wakati anafanya manunuzi.
Amesema mtendaji alimfuata na kumuambia shamba hilo unatakiwa kuongeza Sh milioni mbili alimjulisha hiyo fedha hana na kumuambia akatafute hata Sh milioni 1.5.
"Ilinibidi niwaletee ng'ombe zangu sita ili kulipa hiyo sh milioni 1.5 wakati naanza kulisafisha shamba hilo akaja mtu mmoja anasema eneo ni lake nikamuuliza mtendaji huyu imekuwaje kaja kupanda mazao katika shamba langu akanimbia subiri ila shamba ni lako," amesema.
"Mheshimiwa Makonda naomba unisaidie juzi wameniita wananiambia wanipe Sh. milioni 3.5 ina maana wamejua unakuja ndio wanataka kunirudishia hiyo hela nimewakatalia nimelipa riba hadi imefika zaidi ya milioni tano katika kipindi cha miaka miwili alafu leo wanataka kunirudishia hiyo hela nimewakatalia naomba unisaidie katika hili,"
Amesema viongozi hao wa kijiji humtafuta mtu mbadala kwa ajili ya kuuza maeneo ili wao wasijulikane kama wanacheza michezo hiyo na kusababisha usumbufu kwa wananchi.
Makonda baada ya kusikiliza alihoji iweje mtendaji kuhusika na kuuza viwanja “Kwa hiyo wanampa mtu akauze huku wakijua hilo shamba sio la kwao OCD upo wapi na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mchukueni mtendaji wa kata mkafungue jalada na wote mnaohusika kuzulumiwa mkatoe taarifa,”
“Kama ni mhalifu tutamalizana naye tutawapiga spana mpaka wanyooke nilishasema sitaki watendaji wazembe na wala rushwa,” amesema Makonda.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED