Dk. Samia: Tutaweka nguvu watanzania wabobevu watuwakilishe kimataifa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:59 PM Dec 02 2024
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

“Ndugu zangu, kufuatia msiba huu tumepokea salamu za pole na faraja kutoka sehemu mbalimbali duniani. Viongozi wa Afrika na viongozi wa Kimataifa. Na ninawashukuru wote waliotuma salamu hizo kwa serikali yetu. Nawashukuru pia viongozi wa Kimataifa ambao wameweza kuja kushiriki nasi kumuaga ndugu yetu. Haswa viongozi wa WHO. Muheshimiwa Spika na waombolezaji wenzangu. Mambo mengi yamesemwa kumuhusu ndugu yetu Dkt. Faustine Ndugulile. Tumeyasikia mengi katika fani, katika uongozi. Mchango wake alioutoa kwa jamii na nchi yake kupitia utumishi wake, katika taaluma yake lakini pia katika siasa,”Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.