Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Bara, Isihaka Mchinjita, ameeleza kuwa Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama hicho, Abdul Nondo, amepigwa na kuteswa vibaya, hali inayomfanya ashindwe kuzungumza vizuri.
Nondo anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana jazi alfajiri akiwa katika Stendi ya Mabasi ya Magufuli, iliyopo Mbezi Louis, Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mchinjita, baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa kuwa linaendelea kuchunguza waliomhusisha na tukio hilo, wakiwemo watu waliotumia gari aina ya Land Cruiser nyeupe.
Usiku wa tukio, Nondo alikutwa akiwa ametupwa katika fukwe za Coco Beach, ambapo wasamaria wema walimuokoa na kumpeleka katika makao makuu ya chama hicho. Baadaye, alikimbizwa Hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya matibabu, ambapo bado anaendelea kupatiwa huduma ya afya.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED