Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee amesema Dk.Faustine Ndugulile ametuachia somo la kusimama katika ukweli na kuwa moto kusimamia katika jambo unaloliamini.
“Mimi kama mwakilishi wa kambi ya watu wachache, namfahamu Dk.Ndungulile katika shughuli zetu toka mwaka 2010, alikwua siyo mnafiki, alikua kama ana jambo lake kama ni nyeupe atasema nyeupe kama ni bluu ni bluu.
"Alitumia muda wake kuwakilisha wananchi, alikuwa anasema ukweli tupu pasipokujali itamgharimu vipi"
"Alipata ajali za kisiasa kwa sababu ya kuzungumza ukweli, alikuwa mtii, anatufundisha kwamba hutakiwi kuwa baridi au vuvuvugu inabidi uwe moto utimize ndoto."
"Watoto wake wanajua baba yao ni wa moto na sisi wanasiasa tulijua ni wa moto, hivyo tunaposimama katika jambo la ukweli tunatakiwa tuwe wa mto, ukiwa wa moto unasaidia nchi na kuinua taifa,"amesema Mdee.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED