RAIS Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania itaingia tena kwenye ushindani wa nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika.
"Lakini nisema Dk.Faustine katika safari yake hii ya mwisho ameweka heshima kubwa kwa nchi yetu kwa kupata nafasi ile na niseme kwamba Mungu amechukua amana yake lakini kwetu sisi ni kwenda mbele.
"Tutaingia tena kwenye ushindani wa nafasi ile, tutatafuta Mtanzania mwenye sifa zinazoweza kushindana na ulimwengu, tutaingia tena na tutaweka nguvu ile ile ili kUweka heshima ya nchi yetu.Tunamshukuru sana Dk.Faustine kwa mchango alioutoa kwa taifa,”amesema Rais Samia.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED