WATOTO wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani(WHO), Kanda ya Afrika, Dk, Faustine Ndungulile, wamesema wamepoteza mwanga wao, nguzo na shujaa wao kutokana na vitu alivyokuwa akivifanya kwa familia na kwa jamii.
“Tulipata baba ambaye alikuwa shujaa na aliyetufundisha mambo mengi, kimwili tumempoteza lakini kiroho tutaendelea kuwanaye,"wamesema hivyo Martha na Kelvin.
"Baba alikuwa jasiri, mkarimu, mwenye akili na alipenda watu, nilipata baba...kwangu atabaki kuwa baba bora zaidi,"amesema Melvin.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED