MWANAHARAKATI nguli nchini, Aginatha Rutazaa, ameiomba serikali kuunda Mahakama Maalum, itakayokuwa na jukumu la kushughulikia kesi pekee zinazohusu ukatili wa kijinsia.
Rutazaa, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TUSONGE CDO, amesema kesi hizo kwa sasa zinashughulikiwa katika mahakama za kawaida na mara nyingi hazipati ule uzito wake wa kufanyiwa kazi kwa haraka, kwa ajili ya kusaidia wale waathirika waliofanyiwa matukio hayo.
Alikuwa akizungumzia leo, Desemba 2,2024 siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza Novemba 25 na zikitarajiwa kufikia ukomo wake Desemba 10 mwaka huu.
"Tunajua kesi hizi zinashughulikiwa katika mahakama za kawaida na mara nyingi hazipati ule uzito wake wa kufanyiwa kazi kwa haraka kwa ajili ya kusaidia wale wahanga waliofanyiwa matukio haya.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED