Watendaji wakuu taasisi, mashirika watakiwa kuzitendea haki nafasi zao

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 12:58 PM Oct 09 2024
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Dk. Tausi Kida.
PICHA: CHRISTINA MWAKANGALE
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Dk. Tausi Kida.

WATENDAJI wakuu wa taasisi, mashirika ya umma na wakala wa serikali, wametakiwa kuzitendea haki nafasi za uongozi wa umma walizopewa kuzisimamia, pamoja na kuongeza tija katika utoaji huduma.

Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Moses Kusiluka, ameyasema hayo kwenye hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Dk. Tausi Kida, kwenye ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watendaji wakuu hao, wakiwamo wapya 111, yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Msajili wa Hazina, Taasisi ya Uongozi, pamoja na wadau kutoka sekta ya umma na binafsi.

Awali, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Kadari Singo, amesema kuna changamoto ya kukidhi vigezo vya uongozi miongoni mwa viongozi, huku wengi wao wakiegemea katika uongozi kiutawala na mbinu za ujuzi.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amesema mafunzo hayo ambayo yatafanyika mara mbili kwa mwaka, yanalenga kuwajengea uwezo, uzoefu wakuu hao pia kujitathmini na kuweka mikakati ya kusonga mbe