Benki ya Equity, TFS yapanda miti 10,000

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:15 PM Dec 13 2024
Benki ya Equity, TFS yapanda miti 10,000.
Picha:Mpigapicha Wetu
Benki ya Equity, TFS yapanda miti 10,000.

Benki ya Equity Tanzania, kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imepanda miti 10,000 katika Shule ya Sekondari ya Kirungu, Kijiji cha Kirungu, Wilaya ya Buhigwe, Mkoa wa Kigoma.

Miti iliyopandwa ni aina ya Misindano ya asili (Pines), kwenye eneo la shule lenye ukubwa wa hekta 9.

Lengo la mpango huo wa kupanda miti ni kuhifadhi uoto wa asili na kupunguza athari za mmomonyoko wa udongo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo jana mkoani Kigoma, Mkuu wa Kitengo cha Uendelevu wa Equity, Hellen Dalali alisema, wana lengo la muda mrefu la kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti kila mwaka.

"Hii ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Uimarikaji na Urejeaji Uchumi wa Tanzania (ARRP) chini ya nguzo ya Kijamii na Kimazingira, inayolenga kuimarisha uhimiri wa mazingira na kuchangia maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi kwa jamii zetu," amesisitiza.

Shughuli hiyo  imeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Ngayalina.