MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amesema jamii inapaswa kuwa makini na aina ya mlo, kwa kuwa hata unywaji chai asubuhi, watu wengi hunywa bila kuhisi njaa.
"Chai sio lazima. ‘Breakfast’ maana yake vunja funga. Nakula matunda sita mchana. Au chai kavu, ukiweka tofauti kati ya mlo mmoja Hadi mwingine ndivyo unavyopunguza simu mwilini.
"Unachuja sumu mwilini. Mimi naagiza chai bila sukari au kunywa kahawa, naweza kuanzia mlo saa sita mchana tangu nimekula jana usiku.
Amesema kwamba mara nyingi mtu anakunywa chai asubuhi kwa kufuata utaratibu uliozoeleka, ingawa binadamu huwa haamki na njaa, iwapo alipata mlo usiku.
Bingwa huyo ambaye aliyebobea katika magonjwa ya moyo, ameshauri mambo matano, ikiwamo kila mmoja kufahamu kiwango cha presha yake; kujua uzito ukoje; kujua kiwango cha sukari; na kiwango cha ukubwa wa kiuno chake.
Prof. Janabi, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali hiyo, mafanikio na changamoto katika mwaka 2024 pamoja na matarajio.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED