Serikali imeendelea kuonyesha dhamira ya kimkakati katika kukuza na kuimarisha kada ya ustawi wa jamii ili kuhakikisha inakidhi mahitaji ya maendeleo ya kidigitali, hususan katika masuala ya malezi ya watoto na familia.
Akizungumza katika Mahafali ya 48 ya Chuo cha Ustawi wa Jamii Kampasi ya Kijitonyama na ya saba (7) Kampasi ya Kisangara Kilimanjaro yaliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe jana 11 Desemba 2024, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima, alieleza kuwa Serikali imeweka mkazo mkubwa katika kuhakikisha malezi ya watoto na familia yanaimarika katika zama hizi za kidigitali.
Dk. Gwajima alibainisha kuwa Serikali iko katika hatua nzuri ya kuandaa sheria mahsusi itakayomuwezesha Msajili wa Kada ya Ustawi wa Jamii kusajili wahitimu mara tu wanapomaliza masomo yao, ili waweze kuhudumia jamii kwa viwango vya juu.
“Sheria hii itakwenda kuleta mabadiliko makubwa katika taaluma ya ustawi wa jamii na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Ni hatua itakayosaidia pia kulinda taaluma na kuhakikisha wahitimu wanatoa huduma bora zaidi,” alisema Dk. Gwajima.
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dk. Joyce Nyoni, alieleza kuwa katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 3,121 wamehitimu, ambapo asilimia 65.5 ni wanawake na asilimia 34.6 ni wanaume.
Dk. Nyoni aliongeza kuwa chuo hicho kimepata mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mitaala mipya minne (4) ambayo ni:
Mitaala hii imeidhinishwa rasmi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) na inatarajiwa kuanza kutumika mwaka wa masomo 2025/2026.
Aidha, chuo kinaendelea kuhuisha mitaala yake itakayofikia ukomo wake mwaka 2025/2026 ili iendane na mahitaji ya soko la ajira na kujenga uwezo wa wahitimu kujiajiri.
Mahafali hayo yamekuwa ushuhuda wa hatua kubwa zinazochukuliwa na Serikali pamoja na taasisi za elimu ya juu katika kuhakikisha Tanzania inajipanga ipasavyo kwa maendeleo ya kidigitali. Wahitimu walihimizwa kutumia maarifa yao kuboresha maisha ya jamii wanayohudumia.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED