MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Mohamed Janabi, amesema ni vyema kila mmoja akapunguza kugombana na mtu au watu ili kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza (NCDs).
Amesema miongoni mwa magonjwa hayo ni kisukari na presha, na kwamba yasipodhitiwa huathiri maisha na afya kwa ujumla.
Prof. Janabi, aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali hiyo yakiwamo mafanikio, changamoto katika mwaka 2024 pamoja na matarajio.
“Kuna namna ya kupunguza ‘stress’ (msongo wa mawazo), kuna homoni inayoitwa ‘cortisol’ muda wote ikiwa juu inaongeza na kuwa na sukari, kugombagombana kila siku, inaharibu maisha yako, usilichukulie poa.”
Cortisol ni homoni ya steroid ambayo husaidia mwili kukabiliana na mafadhaiko na hatari.
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED