DC Twange, Saashisha wanogesha serikali mitaa

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 12:47 PM Oct 14 2024
Viongozi wa Wilaya ya Hai, wakiongoza makundi ya wananchi katika michezo mbalimbali, wakati wa bonanza la kuhamasisha uandikishaji wananchi daftari la mkazi

WILAYA ya Hai, mkoani Kilimanjaro, imefanikiwa kuyakutanisha makundi mbalimbali ya jamii, kwa ajili ya kuongeza hamasa ya wanachi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la mpiga kura lililoanza Oktoba 11 mwaka huu.

Uandikishaji daftari la mpiga kura, unafanyika kitaifa na kuendelea hadi Oktoba 20 mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya Hai, Lazaro Twange, akizungumza jana katika viwanja vya Half London na mamia ya wananchi waliojitokeza katika bonanza la uhamasishaji watu kujiandikisha, amewataka waananchi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili wawe na sifa ya kushiriki uchunguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Bonanza hilo lilihusisha michezo mbalimbali, ikiwemo mpira wa miguu, basketball (mpira wa pete), joging, drafti na karata.

"Kwa hiyo jamani msisitiza wangu mkubwa tuwafikishe tunatimiza wajibu wetu wa kizalendo kama Wananchi kwa ajili ya Viongozi watakao tutumikia,"amesema DC Twange.

Katika bonanza hilo, Mbunge wa Hai (CCM), Saashisha Mafue, amesema wanafanya  uhamasishaji kuwambusha wananchi kujitokeza na kwenda kujiandikisha ili kutimiza sifa za kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa. 

"Sote tunafahamu kama mchakato wa maendeleao unaanzia katika serikali za mitaa. Kanuni yetu inatuambia serikali za mitaa ni sauti ya wananchi.

...Hivyo tujitokeze kushiriki ,wale ambao mpo hapa, tafadhali mkajiandikishe, tumuunge mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili uchaguzi huu uweze kufanikiwa.

"Hakikusheni mnapoenda kujiandikisha familia usiisahau pamoja na majirani, viongozi wa kata, endeleeni kuhamasiaha wananchi."