Serikali punguzeni kodi na tozo wachimbaji wasipate vishawishi kutorosha madini

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 06:01 PM Oct 14 2024
Serikali punguzeni kodi na tozo wachimbaji wasipate vishawishi kutorosha madini

WACHIMBAJI wa madini katika mkoani Songwe wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi ya asilimia 2 wanayotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwa asilimia moja ili kupunguza vishawishi vya kutosha madini na kwenda kuyauza kinyemela.

Wamesema hayo leo kwenye maonesho ya wachimba madini yaliyofanyika katika kata ya Saza wilayani Songwe mkoani Songwe ambayo yameandaliwa na  Mc Edwin Luvanda Branding and Entateiment Company.

Meneja Mkuu wa kampuni ya Songwe Gold Family (SGF), Michael  Matoke, amesema kuna tozo na kodi za malimbikizo ya madeni ya nyuma ambayo serikali ilitangaza kuyasamehe lakini katika hali ya kushangaza TRA inaendelea kuwatoza wachimbaji hali inayowafanya washindwe kujua upi ni msimamo wa serikali.

"Suala hili la tozo malimbikizo ya madeni ya nyuma kwa namna moja au nyingine linachangia hata utoroshaji wa dhahabu kwasababu wachimbaji wengine hawana hata mitaji sasa unapompigia mahesabu ya nyuma wakati kwenye akaunti yake hana hata Sh.milioni 20 huyu unamfanya awaze zaidi," alisema.