FRELIMO yatangazwa mshindi kiti cha Urais, upinzani wapinga

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 08:04 PM Oct 14 2024
FRELIMO yatangazwa mshindi kiti cha Urais, upinzani wapinga
Picha;Mtandao
FRELIMO yatangazwa mshindi kiti cha Urais, upinzani wapinga

CHAMA kikongwe cha siasa huko Msumbiji, FRELIMO, kimejipatia ushindi wa kiti cha urais.

FRELIMO, ni miongoni mwa vyama vikongwe barani Afrika na kimedumu mamlakani kwa takribani nusu karne.

Upinzani umepinga matokeo hayo, yaliyotangazwa hivi punde leo, baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 9, mwaka huu.

Nickson Katembo, mchambuzi wa kisiasa akiwa nchini humo anasema wananchi walio wengi hawakutarajia matokeo hayo.

Daniel Chapo, ametangazwa mshindi wa kiti hicho, kupitia chama tawala cha FRELIMO katika uchaguzi huu, akimrithi Rais anayemaliza muda wake, Filipe Nyusi.

Mpinzani wake mkuu ni Ossuo Momade, kutoka chama cha RENAMO. Wagombea wengine walikuwa ni Lutero Simango wa chama cha MDC, na mgombea binafsi Venâncio Mondlane. 

FRELIMO, imedumu madarakani kwa miaka takribani 50.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (CNE), zaidi ya watu milioni 17 wa Msumbiji walijiandikisha  kupiga kura, wakiwamo 333,839 wanaoishi nje ya nchi.

BBC/RFI