Mkusanyiko wa Land Rover Arusha, waupiku wa Bavaria Ujerumani mwaka 2018

By Christina Mwakangale , Nipashe
Published at 07:56 PM Oct 14 2024
Mkusanyiko wa Land Rover Arusha, waupiku wa Bavaria Ujerumani mwaka 2018
Picha: Mtandao
Mkusanyiko wa Land Rover Arusha, waupiku wa Bavaria Ujerumani mwaka 2018

TAKRIBANI magari 1,034 aina ya Land Rover, yamekutanishwa jijini Arusha, ikiwa ni idadi mara mbili ya Ile iliyotokea mwaka 2018.

Mwaka 2018 katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani, kulikuwa na mkusanyiko wa magari 632 ikiweka rekodi ya dunia na iliyotambuliwa na Guinness.

Sasa, mji wa Arusha, leo umefanikisha mkusanyiko huo kuuzidi wa Bavaria. Lengo ni kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ambaye leo ametimiza miaka 25 tangu afariki dunia.

Madereva wa magari ya aina ya Land Rover kutoka mikoa tofauti nchini wamekusanyika Arusha, kaskazini mwa Tanzania kwenye tamasha maalumu lenye lengo la kuvunja rekodi mpya ya dunia.

Tamasha hilo la siku tatu, limehitimishwa leo, Jumatatu Oktoba 14.

Rekodi ya sasa ya dunia ya mkusanyiko wa magari mengi ya Land Rover kwa mujibu wa kitabu cha Guinness ni ya mwaka 2018 ikishikiliwa na jimbo la Bavaria, yakitengeneza msafara uliofikia umbali wa kilometa 7.4

BBC Radio