BARANI Afrika mabadiliko ya kisiasa iwe kwa mapinduzi au ya mfumo rasmi kupitia upigaji kura, yamepamba moto, kuanzia Botswana hadi Senegal wananchi wamefanya ‘jambo lao.’
Karne ya 21 inaweka rekodi zaidi kwa bara hili la kuleta mabadiliko ya kisiasa huku baadhi ya vyama vilivyodumu hata nusu karne vikiondoshwa madarakani.
Upepo wa mabadiliko haupo Afrika pekee na safari hii nchini Syria dunia imeshuhudia raia wakiingia, kupiga picha huku wakichukua chochote watakacho, wakidai ni kulipiza kisasi kwa miaka mingi ya ukandamizaji na umaskini kwa sababu ya Bashar al-Assad na baba yake.
Wakazi wa maeneo tofauti ni mjini Damascus wameelezea namna walivyokuwa wakisubiri kwa wasiwasi habari juu ya kile kinachotokea katika mji mkuu wa Syria usiku kucha.
Baada ya saa kadhaa za ripoti za waasi walikaribia zaidi na zaidi, vikosi vilitangaza kuwa Damascus ni ‘huru’ mbali na mtawala wa muda mrefu Bashar al-Assad mapema Jumapili.
Video mitandaoni kwenye vyombo vya kimataifa kama BBC, zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha watu wakishangilia barabarani na kuwakaribisha wapiganaji hao waasi, pamoja na wafungwa wakiachiliwa huru kutoka katika gereza la Saydnaya.
“Hakuna mtu aliyelala nchini Syria usiku huo ... hakuna Msyria aliye ng'ambo aliyelala," Rania Kataf, ambaye anaendesha ukurasa wa Facebook wa Humans of Damascus, anasema.
“Jamii nzima ilikuwa imeshikilia simu zao zikisubiri habari za mwisho. Ninahisije? Kuzidiwa... Sote tunahisi kama tumekuwa chini ya maji, kwa miaka 13 na sote tulipumua.”
"Najua kwamba kuna watu wengi ambao ni wakubwa zaidi kuliko mimi ambao wamepitia mengi sana." Anasema kwa hisia mchanganyiko, hata hivyo tangu mashambulizi ya makundi ya waasi yaanze, lakini hakuwa na hofu tena.
Danny Makki, mwandishi wa habari anayeishi Damascus, anaelezea matukio ya Jumapili wiki iliyopita, huko Umayyad, ambako ni nyumbani kwa mashirika muhimu ya serikali, ikiwa ni pamoja na Wizara ya Ulinzi na Vikosi vya Wanajeshi vya Syria.
"Watu walikuwa wakifyatua risasi hewani, watu walikuwa wakicheza, kupiga picha na kulia," anasema mwandishi huyo.
"Nilizungumza na askari kutoka kwa wanamgambo. Mmoja anasema alikuwa akijiandaa kwa hili kwa muda mrefu. Hakuwa akishiriki katika mashambulizi ya Aleppo, lakini alipoona waasi wakiwasili viunga vya Damascus, ndipo alipochukua silaha."
Anasema baadhi ya wapiganaji hao waasi walikuwa wakitumia magari ya Jeshi la Syria yaliyotelekezwa.
"Nilipokuwa nikiendesha gari kuzunguka Damascus, niliona wanajeshi wa Syria wakitembea wakiwa katika nguo za kiraia barabarani, bila kujua wapi pa kwenda."
“Wasiwasi wa watu ulikuwa usalama, na kuhakikisha kuwa hakuna mapigano ndani ya safu ya upinzani."
“Kwa mara ya kwanza kabisa, kuna hisia za kweli za uhuru. Tunachohisi kinafanana sana na tulivyohisi wakati wa mapinduzi yalipoanza mwaka wa 2011. Huu ni mwendelezo wa ndoto ambayo ilikuwa imeanza mwaka huo."
Mwandishi huyo anasema kuwa Wasyria wanahisi hofu na wasiwasi juu ya siku zijazo, lakini "leo, watu wote wa Syria watasherehekea tu."
Mtangazaji huyo wa televisheni ya taifa anasema viongozi wa upinzani wamehakikisha usalama wa vituo vya kijeshi vya Russia na balozi za kidiplomasia katika eneo la Syria.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, inasema kuwa kambi hizo nchini Syria zimewekwa katika hali ya tahadhari, lakini inadai kuwa hakuna tishio kubwa kwao kwa sasa.
NANI ANAMSHTAKI ASSAD
Bashar al-Assad alikuwa mshirika mkuu wa Russia katika Mashariki ya Kati. Kremlin au ikulu ya Urusi ilikuwa imewekeza sana kwake.
Mamlaka ya Russia, ikajitahidi kukubali kupinduliwa kwake lakini kama pigo kubwa kwa upande wa Moscow.
Siku ya Jumapili usiku kipindi cha televisheni cha taifa cha Russia cha kila wiki kililenga jeshi la Syria, kikililaumu kwa kutopigana dhidi ya waasi.
"Kila mtu aliweza kuona kwamba hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya kwa mamlaka ya Syria," mtangazaji Yevgeny Kiselev akasema.
"Lakini huko Aleppo, kwa mfano, maeneo yaliachwa bila vita vyovyote. Maeneo yenye ngome yalisalimishwa moja baada ya jingine na kisha kulipuliwa, licha ya wanajeshi wa serikali kuwa na vifaa bora zaidi na kuwazidi washambuliaji mara nyingi. Inashangaza.”
Mtangazaji huyo anadai kwamba Russia, daima ilikuwa na matumaini ya upatanisho nchini Syria.
"Bila shaka hatujali kile kinachotokea Syria. Lakini kipaumbele chetu ni usalama wa Russia yenyewe, kile kinachotokea katika ukanda wa Operesheni Maalum ya Kijeshi (vita vya Urusi nchini Ukraine)."
Licha ya miaka tisa ya Russia, kumwaga rasilimali katika kumweka Bashar al-Assad madarakani, Warusi, wanaambiwa wana mambo muhimu zaidi ya kuhangaikia, si jambo lake.
ALIKO SASA
Rais huyo aliyepinduliwa yuko Moscow na familia yake baada ya Urusi kuwapa hifadhi kutokana na sababu za kibinadamu.
Jumapili usiku na ikulu ya Kremlin, ilisisitiza kuwa makubaliano yamefikiwa, ili kuhakikisha usalama wa kambi za kijeshi za Urusi nchini Syria.
Awali Moscow ilisema kambi hizo ziko katika tahadhari kubwa lakini hakukuwa na kitisho dhidi yao kwa sasa. Assad ameikimbia nchi baada ya waasi kuchukua udhibiti wa mji mkuu Damascus huku akitoa maagizo kwamba ukabidhi wa madaraka ufanyike kwa amani.
Rais wa Marekani, Joe Biden, anasema ni lazima Assad awajibishwe kwa vitendo vya mauaji na mateso kwa mamia ya maelfu ya Wasyria. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litafanya hivi leo mkutano wa dharura na wa faragha ili kuijadili hali inayoendelea nchini Syria.
ASSAD
Bashar Hafez al-Assad, ana miaka 60 akizaliwa Septemba11, mwaka 1965, akiwa mwanasiasawa Syria ambaye aliyeanza kuongoza taifa hilo Julai 17, 2000.
Alikuwa kamandamkuu wa Jeshila Siria na Katibu wa Mkoa wa tawila Chama cha Waajemi la Ba'ath nchini Syria, baba yake, Hafez al-Assad, alikuwa Rais wa Syria kutoka mwaka 1971hadi 2000.
BBC
© 2024 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED