Wanajeshi majeruhi 200 wakiwamo Watanzania warejea nchini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:14 PM Feb 25 2025
Bendera za nchi wanachama SADC
Picha: Mtandao
Bendera za nchi wanachama SADC

WANAJESHI 200 wakiwamo Watanzania, wanaohitaji huduma ya matibabu walioko katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), kwa ujumbe unaojulikana kwa jina la SAMIDRC, wameondoka Goma kuelekea Kigali, kupata ndege kuwarejesha makwao.

Magazeti ya Rwanda yanaripoti kuwa wanajeshi 129 wanatoka Afrika Kusini, 40 kutoka Malawi na 25 kutoka Tanzania.

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini alitangaza hayo wikiendi iliyopita kwamba wanajeshi wao waliojeruhiwa katika mapigano na M23 nchini DRC wataanza kurejeshwa makwao wiki hii.

Donatien Mugabo, mkazi wa Gisenyi nchini Rwanda, ambaye ameshuhudia magari yaliyokuwa yamewabeba askari hao yakiondoka mpakani kwa upande wa Rwanda, ameiambia BBC kuwa walikuwa kwenye mpaka huo kwa saa kadhaa.

Mwanajeshi
Walifika mpakani Jumatatu (jana) saa sita mchana na waliondoka mpakani baada ya saa 12 jioni, Donatien anasema.

Haijabainika ni nini kilisababisha wacheleweshwe mpakani. Vyombo vya habari vya Goma, linalodhibitiwa na M23 na nchini Rwanda vilipigwa marufuku kupiga picha au kuzungumza na wanajeshi, kama ilivyokuwa wakati mamluki wa Ulaya walipoondoka Goma kupitia Rwanda.

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na nchi walikotoka askari hao hawajazungumzia kuachiliwa kwa askari hao wanaotajwa kuhitaji matibabu.

BBC