WALE mnaokopa kwenye mtandao ya simu na kubadilisha laini za simu, ili kukwepa kulipa deni, wameambiwa wabaini kuna kanzidata ya kumbukumbu ya madeni ya wateja wote mtandaoni, ambao hukosa mikopo kwenye taasisi nyingine za fedha.
Hayo yamesemwa na BoT wakati wakiwasilisha mada mbalimbali kuhusu sera ya fedha, kwa waandishi wa habari Februari 25, 2025 mjini Mtwara.
“Kumekuwa na tabia ya mtu anataka kumtumia mtu fedha Sh. 500 alafu umepungukiwa Sh. 50 unakopeshwa na mtandao wa simu, inapita miezi hadi 10 hujalipa, taraifa zako zinapelekwa kwenye kanzidata kwamba ni mkopoaji asiyelipa yaani mkopo chechefu.
“Muda umepita unakwenda benki unaomba mkopo wanaingia kanzidata ya ‘Credit Reference Bureau’ wakiingiza jina lako mara moja unaonekana hukulipa Sh. 500 na deni limekuwa na riba, moja kwa moja watakwambia nenda BoT”.
Imefafanua kuwa mlolongo wake ni mrefu kwa kuwa hadi mteja aende BoT, ili akakusafishe unapokopa ni benki inakukopesha na si mtandao. Wananchi wanapokopa wawajibike kulipa hata kama ni fedha ndogo, suluhisho si kuhama mtandao,” amesema.
“Sh. 500 inakukosesha kukosa mkopo kutoka benki. Usipolipa kwa wakati jina litatokea kuwa wewe ni mdeni sugu, hustahili kukopeshwa,” amesema.
“Wananchi wajue, hata mikopo midogo midogo inapelekwa Credit Reference Bureau, tuuelimishe watu kuna watu wanakopa hawalipi wanaobadilisha laini ya simu haisaidii kitu.
Siku unaenda kuomba mkopo wanakukatalia, kumbe ni kutokana na tabia ya kukopa na kutokurejesha kwenye kampuni za simu kunakunyima haki nyingine,” amefafanua Ofisa kutoka Kurugenzi ya Tafiti na Sera za Uchumi, Dominic Mwita akiwasilisha mada ya mfumo wa utekelezaji wa sera ya fedha kwa njia ya riba iliyoanza Januari 2024.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED