WANAFUNZI 121 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wameondolewa masomoni baada ya kupatikana nah atua ya kuhusika kuchezea mfumo wa matokeo(SR2) Mwaka 2023/24.
Taarifa hiyo imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Masoko UDOM, kufuatia kusambaa mitandaoni taarifa madai ya wanafunzi 400 kufutwa masomo kwa tuhuma za kudukua mfumo.
Kwa mujibu wa Kitengo hicho, wanafunzi 170 walituhumiwa kuchezea mfumo huo na serikali iliunda kikosi kazi kwa ajili ya kuchunguza tuhuma hizo na kutoa wito kwa watuhumiwa kufika kusikilizwa kabla ya kutoa maamuzi.
Wanafunzi 148 walisikilizwa, wanafunzi 32 hawakufika kusikilizwa na kati ya waliosikilizwa 121 walikutwa na hatia na kesi za wanafunzi 15 zinaendelea na uchunguzi zaidi huku wawili hawakukutwa na hatia.
Hata hivyo, kwa mujibu wa taratibu za Chuo hicho mwanafunzi ambaye hajaridhika na maamuzi ya seneti anapewa nafasi ya kukata rufaa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED