Abiria alivuruga utaratibu na kuwashambulia wafanyakazi wetu-UDART

By Salome Kitomari , Nipashe
Published at 08:12 PM Feb 25 2025
Abiria wakimbilia kupanda gari.
Picha:Maktaba
Abiria wakimbilia kupanda gari.

KAMPUNI ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART),imesema tukio la mashambulizi lililotokea Februari 25,2025 katika Kituo cha Kimara Temboni lilihusisha abiria kuwashambulia wafanyakazi wao waliokuwa kazini.

Akizungumza na Nipashe Digital kwa njia ya simu, Ofisa Mawasiliano wa UDART, Gabriel Katanga, amesema:

"Abiria huyo alivunja utaratibu kwa kuwapita wengine waliokuwa kwenye foleni, hali iliyozua vurugu kati yake na abiria wengine waliotaka afuate utaratibu. Wafanyakazi wetu walijaribu kumzuia na kumtaka apange foleni, lakini badala yake aliwashambulia."

Ameeleza kuwa katika shambulio hilo, wafanyakazi wawili wa UDART walijeruhiwa, mmoja akipata majeraha mkononi na mwingine sehemu mbalimbali za mwili.

Katanga amesema kuwa tukio hilo limesharipotiwa polisi na tayari jalada la kesi limefunguliwa chini ya kumbukumbu namba KIM/RB/513/025 likihusiana na shambulio la mwili.

Kama ulipitwa na habari hii Kliki hapa.