Gambo: Milioni 200 zilitaka kutafunwa na mafisadi Arusha

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 10:37 AM Feb 25 2025
@nipashedigital MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema serikali imeokoa kiasi cha zaidi ya Sh. million 200 zilizotaka kupigwa na baadhi ya watu jimboni hapo wakati wa ununuzi wa eneo la shule kwenye Mtaa wa Mashariki Kata ya Muriet. #fypシ゚ #mrright #kenyatiktok_kenya🇰🇪💖 #tanzaniatiktok #videoviral #Tanzania #fyviral #for #Simba #Azam #For #Nipashe #NipasheMwangaWaJamii #Raissamia ♬ original sound - Nipashe Digital
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo.

MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema serikali imeokoa kiasi cha zaidi ya Sh. million 200 zilizotaka kupigwa na baadhi ya watu jimboni hapo wakati wa ununuzi wa eneo la shule kwenye Mtaa wa Mashariki Kata ya Muriet.

Mbunge huyo ameyabainisha hayo leo jimboni hapo, huku akiwashukuru Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kusimama kikamilifu, kupambana na kufanikiwa kuzuia ufisadi huo.

"Rais Samia Suluhu Hassan anatafuta fedha kila mahali ili kuwasaidia wananchi wa Jiji la Arusha lakini kuna wajanja wachache wameungana ili kupiga dili. Mimi nimepewa dhamana na wananchi wenzangu ya kulinda msitu na najua kuna gharama zake ambazo nipo tayari kuzibeba," amesema Gambo.

Naye, Diwani wa kata ya Ngarenaro Isaya Doita ameunga mkono msimamo huo wa Gambo kwa kusema "Manyang’au' wameshindwa na sasa shule itajengwa”.

Aidha, wananchi wa Mtaa wa Muriet Mashariki wameishukuru serikali ya Rais Samia kwa kuwanunulia eneo la kujenga shule kwakuwa itasaidia kuondoa changamoto ya watoto wao kusafiri umbali mrefu kufuata masomo.