UCHUNGUZI uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Bodi ya Shule ya Sekondari ya Geita, umewatia hatiani na kuwafukuza shule wanafunzi saba kwa kuratibu vurugu, zilizizofanyika hivi karibuni wakishinikiza mwanafunzi aliyesimamishwa masomo kurejeshwa shule.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi (SACP), Safia Jongo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari na kueleza kuwa walichukuliwa wanafunzi 71 kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo lililofanyika Februari 20, 2025.
Pia amesema kati ya wanafunzi hao 71, wanafunzi 19 wamesimamishwa shule hadi Mei 5, 2025 huku wanafunzi wengine 45 wakisimamishwa shule kwa muda wa siku 21.
Kamanda Jongo, amesema Februari 21, 2025 jshi hilo, liliwashikilia wanafunzi 30 wa kidato cha sita wa shule hiyo iliyopo Manispaa ya Geita, kwa tuhuma za kufanya vurugu shuleni hapo.
Amesema baadaye walishikilia wengine 41 na kufanya idadi ya wanafunzi hao kufikia 71 na kuwa uchunguzi huo umekamilika, kwa kushirikiana na bodi ya shule.
“Kati ya wanafunzi hao 71 waliobainika kuhusika kwenye tukio hilo, wanafunzi saba wamefukuzwa shule baaada ya kukutwa na hatia ya kuhamasisha vurugu hizo,” amesema Jongo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED