Serikali inaendelea kubuni mbinu kukabiliana na wanyama wakali- Rais Samia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:33 PM Feb 24 2025
Rais Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu huku akiiielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia namna ya kupitia upya kanuni za malipo ya kifuta jasho,machozi.

Ameyasema hayo leo Februari 24,2025 katika ziara alipokuwa akizungumza na wananchi Lushoto Mjini mkoani Tanga 

"Tunaendelea kuongeza Askari Wanyamapori na kubuni mbinu mbalimbali za kufukuza wanyama wakali na waharibifu ikiwemo kutumia ndegenyuki(drones)" Rais Samia amesisitiza.

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana, Naibu Waziri, Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk.  Hassan Abbasi pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.