ZAIDI ya wanawake 800 kutoka maeneo mbalimbali nchini, watayatumia maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, kufanya utalii wa ndani katika vivutio vya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).
Maadhimisho hayo yatakayofanyika mkoani Arusha, Machi 8 mwaka huu, yataongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Jana, Kamishina Mwandamizi Msaidizi wa Huduma za Utalii na Masoko wa NCAA, Mariam kobelo, alisema safari hiyo inatarajia kufanyika Machi 7 mwaka huu, ambayo ni siku moja kabla ya maadhimisho hayo.
Alisema kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, imeandaa safari kwa wanawake waliopo ndani na nje ya mkoa wa Arusha, kwa lengo la kuwapa motisha wanawake wawe na utaraibu wa kutembelea hifadhi zao pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii wa ndani.
"Rais amekuwa kinara wa kuutangaza utalii kupitia filamu mbili ya Tanzania, The Royal Tour pamoja na Amazing Tanzania. Sisi kama wanawake katika uhifadhi na utalii tunaziunga mkono juhudi zake, kwa kuwahamasisha wanawake wote waweze kutembelea hifadhi," alisema Mariam kobelo.
Aidha, alisema wanawake katika mamlaka hiyo wameandaa shughuli nyingine za kimaendeleo katika maadhimisho hayo ni pamoja na kufanya usafi katika barabara wanazopita watalii pamoja na kurejesha shukrani kwa jamii ikiwemo tumbelea wagonjwa waliopo hospitalini kuwapa faraja vijana.
Kwa upande wake, Mkugenzi Mtendaji wa Kampuni yaTanzanite Coparates, Elina Mwangomo, alisema kuwa kampuni yake ndio imeanda ziara hiyo kwa kuahirikiana na mamlaka ya hifadhi ha ngiringiro ambapo safari itagharimu Sh. 170,000 kwa ajili ya usafiri ,kingilio, kofia ,chai ,chakula cha mchana pamoja fedha za waongoza watalii.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED