Tshisekedi kuunda serikali ya umoja kitaifa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:28 PM Feb 24 2025
RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi
Picha: Mtandao
RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi, ataanzisha serikali ya umoja wa kitaifa.

Taarifa kutoka Msemaji wa Ofisi ya Rais, inasema.

Hatua hiyo inakuja wakati kiongozi huyo akikabiliwa na shinikizo la ndani kuhusu jinsi anavyoshughulikia shambulio la waasi wa M23, wanaoungwa mkono na Rwanda, katika mikoa ya mashariki mwa nchi hiyo.

Kushikiliwa kwa maeneo makubwa ya Congo Mashariki na madini yenye thamani na waasi wa M23, kumeongeza hofu ya vita vikubwa zaidi na kuamsha utabiri wa wazi kutoka kwa baadhi ya wawakilishi wa upinzani wenye migawanyiko kuwa utawala wake hautadumu.

Jumamosi, Tshisekedi alisema: "Lazima tuungane ... tusimame pamoja kukabiliana na adui."

Msemaji wa Rrais, Tina Salama, alisema kuwa Tshisekedi ataunda serikali ya umoja wa kitaifa na kufanya mabadiliko katika uongozi wa muungano huo, bila kutoa maelezo zaidi.

Mmoja wa wapinzani nchini humo, Herve Diakiese, akikosoa jitihada za kuunda serikali ya umoja. "Tshisekedi anajali zaidi kuokoa mamlaka yake, wakati sisi tunajali zaidi kuokoa Congo, jambo ambalo linaweza kufanikiwa chini yake au bila yeye," alisema Diakiese, akiongeza kuwa majaribio hayo yamechochea ukosoaji juu ya mkakati wa kijeshi wa mamlaka katika mikoa ya Kivu.

BBC